Thursday, March 21

On 3:49 PM

Pamoja na kuwa aliipata pikipiki yake iliyopotea kwa Lulu, bado Cheche ameendelea kukwepa maswali ya kufedhehesha ya mkewe na familia ya jinsi alivyoipoteza pikipiki yake -- na kwa kuzaliwa mtoto Tea, hali ya taharuki inatanda kati ya Cheche na Cheusi, hasa pale mama Cheche anapowasili bila taarifa na kuzuka mikwaruzano midogo midogo kati ya mama hawa wawili. Mwanaidi naye anamtupia jicho Cheche kwenye arobaini. Je ana wasiwasi kuwa kuna jambo mkwewe anataka kufanya?

Stephen, mdogo wake Duma, naye pia anajiingiza matatani katika mahusiano na msichana mmoja kwenye maskani. Msichana 'anagawa' zaidi ya machungwa
Pata kuitazama uone hali halisi ya nini kinachoendelea...!

0 comments:

Post a Comment