Wednesday, April 24

On 12:14 PM
Shujaa wa taifa anageuka adui wa jamii pale anapoamua kutoboa siri yake. Gilbert Josamu, mwanamasumbwi bingwa wa uzito wa kati, aligundua kuwa ameathirika na VVU wakati akiwa kileleni mwa umaarufu wake. Akiwa anaishi katika jamii ambayo mtu kuwa na VVU ni kama dhambi isiyosameheka, Josamu anaamua kuendelea na ndondi bila kuweka wazi hali yake. Miezi michache kabla hajafariki, Josamu aliamua kuuweka wazi ukweli kuwa amekuwa akiishi na VVU kwa miaka 14. Hivyo pambano gumu kuzidi yote maishani mwake ndo linaanza -- pambano la kusamehewa na kukubaliwa tena.

0 comments:

Post a Comment