Tuesday, July 1

On 8:42 AM
Fareed Kubanda, Wa Kipekee, One of a Kind au kama anavyofahamika kwa wengi Fid-Q, Msanii Mkongwe wa Hip Hop Tanzania mwenye mafanikio makubwa ana machache ya kusema. Msanii alieipandisha Mwanza katika ramani ya kimuziki Tanzania, na mshahiri mahiri mwenye tenzi zenye uzito katika lugha adhimu ya Kiswahili.
Miaka saba bila kushinda tuzo yoyote pamoja na kuteuliwa, na almanusra akate tama, anatukumbusha kuwa mvumilivu hula mbivu. 
Fareed anatukumbusha machache kuhusu changamoto ya kujenga familia akitolea mfano mahusiano ya wazazi wake. Fid Q pia anatueleza ni jinsi gani malezi yake yamempa funzo katika jinsi anavyotarajia kumlea mwanawe.
Fid Q ana mengi ya kutushirikisha kuhusu alichofanya kukuza sanaa na vipaji, jinsi gani tutawatambua wale waliopiga hatua na kuitambulisha nchi kisanii. Ni mmoja wa wasanii waliokomaa, na hekima zikitiririka kinywani kwake....msikilize mwenyewe, upate machache!

0 comments:

Post a Comment