Kupita jitihada na ushirikiano mkubwa, Neria na mume wake Patrick wanajitengenezea maisha waliokuwa wakiyataka siku zote. Lakini Patrick anapofariki katika ajali ya gari, maisha ya Neria yanagueka ghafla na kuwa mateso. Wakati Neria anaomboleza kifo cha mume wake kijijini, shemeji yake, Phineas, yuko mjini akishughulika kumnyang'anya mali zake zote. Phineas anadai kuwa mila za Kiafrika zinampa haki ya kurithi mali zote za kaka yake marehemu. Neria anashuku lengo halisi la shemeji yake, lakini Phineas anapowateka watoto wake, ndipo Neria anaamua kumpiga vita.
Hii ni filamu ya Kiafrika ambayo imegusa watu wengi barani, na inayoshirikisha nyimbo za mwanamuziki mahiri kutoka Zimbabwe, Oliver Mtukudzi.
Filamu hii imeshinda tuzo 10 za kimataifa, zikiwemo tuzo ya OAU Carthage (Egypt) mwaka 1991 na tuzo za MNET nchini Africa Kusini za Muigizaji Bora wa Kike na Filamu Bora mwaka 1992.
0 comments:
Post a Comment