Katika onyesho la mwisho la msimu wa kwanza, kisasi ni kitamu kwa Farida pale anapotonywa habari nyeti toka kwa fundi cherehani, Furaha.
Wakati Mwanaidi anamkabili mkwewe kuhusiana na picha chafu alizompiga Lulu, Cheche anajitetea kwa nguvu kuwa hana kosa.
Wakati fulani Duma anakumbana na Nusura mja mzito akielekea kliniki. Hawezi kuvumilia kumwona akiwa na Mzee Kizito.
Kipindi hiki, Nusura anapata habari ambazo zitayabadilisha maisha yake milele. Na kule kwenye studio ya picha, umbo kutoka nyakati zilizopita, linaibuka kutokea kusikojulikana na kuutikisa ulimwengu wa Cheche.
0 comments:
Post a Comment